» »Unlabelled »

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali itahakikisha viwanda vinajengwa kwa wingi nchini kwani ndiyo msingi imara wa ukuaji wa uchumi na mwarobaini wa tatizo la ajira hususan kwa vijana.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo juzi wakati akikagua ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha Goodwill Tanzania Ceramic katika Kijiji cha Mkiu wilayani Mkuranga, Pwani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Frank Yang alisema jumla ya ajira 4,500 zinatarajiwa kutolewa kiwandani hapo mara ujenzi utakapokamilika.
Akifafanua kuhusu ajira hizo, Yang alisema ajira 1,500 zitakuwa rasmi na zisizo rasmi zitakuwa 3,000 huku wakazi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka kiwanda hicho wanatarajiwa kupewa kipaumbele, katika kiwanda hicho ambacho ujenzi wake utagharimu Dola za Marekani milioni 100 na utafanyika kwa awamu mbili.
Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
“Ujenzi wa kiwanda hiki utainua ukuaji wa uchumi nchini Tanzania kwani utakapokamilika serikali itakusanya shilingi bilioni 30 kwa mwaka ikiwa ni mapato ya kodi,” alisema.
Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuchagua sekta ya viwanda kuwa ndiyo kipaumbele chake katika kukuza uchumi.
Alisema mbali ya ujenzi wa kiwanda cha vigae katika eneo hilo, pia wawekezaji hao kutoka nchini China wanatarajia kujenga viwanda vya mbolea, karatasi na bilauri.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 500 yenye thamani ya Sh milioni 40 ambayo yalitolewa na Balozi wa China nchini, Dk Lu kwa ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Goodwill Tanzania Ceramic, Yang.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...