Watu takriban 50 wauawa katika shambulio Pakistan
Washambuliaji wenye silaha wameshambulia kituo kimoja cha mafunzo ya polisi katika mji wa Quetta huko Pakistan
washambuliaji
sita waliingia katika mabweni ya wanafunzi wa kituo hiko na
kuwashambulia, mamlaka zinasema kuwa watu takribani 50 wameuawa
wakiwemo wanafunzi wa kituo hiko na walinzi, huku wengine wakijeruhiwa.Majeruhi walepelekwa katika hospitali za ndani.
Mamia ya wanafunzi waliokolewa kutoka Chuo cha polisi cha Balochistan wakti wanajeshi walipowasili kupambana na washambuliaji hao.
Washambuliaji wanne wameripotiwa kuuwawa katika makabiliano na jeshi pamoja na polisi, hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulio hilo.
Sauti za milio ya milipuko na risasi zilikua zikisika vizuri, alisema shuhuda mmoja wa tukio hilo.
"walikua wakikimbilia katika majengo yetu huku wakifyatua risasi, sisi tulikimbilia juu na baadae kuruka chini ili kuokoa maisha yetu'' mkufunzo wa kituo hiko aliimbia televisheni ya Geo.
Mwezi nane watu 88 waliuawa katika mashambulio tofauti ya mobamu yaliyolenga hospitali na wanasheria huko Quetta.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:
Post a Comment