» »Unlabelled » UN yataka muda wa amani kuongezwa Yemen

UN yataka muda wa amani kuongezwa Yemen


Umoja wa Mataifa unataka pande husika kuongeza muda wa kusitishwa kwa mapinganoImage copyrightREUTERS
Image captionUmoja wa Mataifa unataka pande husika kuongeza muda wa kusitishwa kwa mapingano
Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zinazozozana nchini Yemen kuongeza muda wa usitishwaji mapigano kwa siku tatu zaidi.
Mjumbe maalum, Ismail Ould Cheikh Ahmed, amesema muafaka wa awali wa kusitisha mapigano ulikuwa wa kutoa fursa kwa Umoja wa Mataifa kutoa misaada ya chakula na huduma za dharura katika maeneo ambayo hayakuweza kufikiwa.
Amesema mapigano yamesitishwa tofauti na ripoti kwamba makubaliano hayo yamekiukwa na pande zote mbili.
Serikali ya Yemeni kwa ushirikiano na vikosi vinavyoongozwa na Saudia,imekuwa ikipigana na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, tangu mwaka 2014 katika juhudi za kuthibiti taifa hilo.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles