» »Unlabelled » Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani

Mataifa yenye wanafunzi werevu zaidi duniani


University of SydneyImage copyrightREUTERS
Image captionWanafunzi wa chuo kikuu cha Sydney, Australia
Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?
Jambo la kushangaza ni kwamba orodha hii inaonyesha taswira tofauti sana na ile inayotolewa na utathmini wa vyuo vikuu.
Shirika la Kimataifa la Uchumi na Maendeleo (OECD) limefanya wazi matokeo ya mtihani wa kupima uwezo wa wanafunzi wanaohitimu kutoka nchi mbalimbali.
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu hutawaliwa na vyuo vikuu kutoka Marekani na Uingereza kama vile Harvard, MIT, Stanford, Oxford, Cambridge na UCL.
Lakini baada ya OECD kuchunguza uwezo wa kusoma na kuandika miongoni mwa wahitimu kutoka vyuo vikuu, wanafunzi walio bora zaidi ilibainika wanatoka Japan na Finland na wala si Marekani na Uingereza..
Nchi zenye wanafunzi bora zaidi wanaohitimu kwa mujibu wa OECD
  1. Japan
  2. Finland
  3. Uholanzi
  4. Australia
  5. Norway
  6. Ubelgiji
  7. New Zealand
  8. England
  9. Marekani
  10. Jamhuri ya Czech
Nchi hizi zote huwa mara nyingi hazina chuo haka kimoja kinachokuwa kwenye orodha ya vyuo vikuu 10 bora duniani.
Badala ya vyuo vikuu vya Marekani kufana, yamkini vyuo vikuu vya Norway na Australia vina wanafunzi bora wanaohitimu.
Kwa mujibu wa orodha ya ubora wa vyuo ya QS World University Rankings, kulikuwa na vyuo 32 vya Marekani katika 100 bora, na chuo kikuu kimoja pekee kutoka New Zealand.
Lakini ripoti ya OECD inaonesha wanafunzi wa New Zealand wanafanya vyema kushinda wenzao Marekani.
Oxford UniversityImage copyrightISTOCK
Image captionOxford kilirodheshwa kuwa chuo kikuu bora duniani kwenye orodha ya gazeti la Times
TokyoImage copyrightISTOCK
Image captionWanafunzi waliohitimu kutoka Japan walifanya vyema zaidi tathmini ya OECD
Orodha ya ubora wa vyuo vikuu ya QS 2016-17
  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford University
  3. Harvard University
  4. University of Cambridge
  5. California Institute of Technology (Caltech)
  6. University of Oxford
  7. University College London
  8. ETH Zurich
  9. Imperial College London
  10. University of Chicago
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles