» »Unlabelled » Mambo saba ambayo ni marufuku Ethiopia

Mambo saba ambayo ni marufuku Ethiopia


Ghasia za hivi karibuni zimejiri kufuatia mauaji ya watu 55 katika tamsaha la kidini la OromiaImage copyrightREUTERS
Image captionGhasia za hivi karibuni zimejiri kufuatia mauaji ya watu 55 katika tamsaha la kidini la Oromia
Serikali ya Ethiopia imetangaza miezi sita ya hali ya tahadhari kufuatia wimbi ambalo halikutarajiwa la maandamano na ghasia.
Wanaharakati katika eneo la Oromia wamekuwa wakifanya maandamano tangu November mwaka jana, na waandamanaji kutoka eneo la Amhara wamejiunga kati.
Vifo vya watu 55 katika tamasha la kidini la Oromo mnamo Oktoba 2 yalisababisha ghasia kuzuka upya, ikiwemo kulengwa kwa biashara za raia wa mataifa ya nje.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema watu 500 wamefariki katika maandamano hayo kwa jumla na wiki iliopita waziri mkuu Hailemariam Desalegn amesema huenda idadi hiyo ikawa ya sawa.
Hali hiyo ya tahadhari ilitangazwa mapema mwezi huu lakini serikali sasa imeeleza wazi ina maana gani kihalisia:
Hizi ndio baadhi ya marufuku:
1. Mitandao ya kijamii
Wanaharakati wametumia simu zao kusambaza taarifa kuhusu maandamano yaoImage copyrightAP
Image captionWanaharakati wametumia simu zao kusambaza taarifa kuhusu maandamano yao
Hakuna ruhusa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, kuwasiliana na serikali inayowaita "vikosi vya nje". Jaribio lolote la kuwasiliana na "makundi ya kigaidi na makundi yanayopinga amani yanayotajwa kuwa ya kigaidi" ni marufuku.
Waandamanaji wametuma ujumbe na video walizo rekodi kwa simu zao katika mitandao ya kijamii na mitandao inayoendeshwa na raia wa Ethiopia walio katika nchi za nje.
Serikali imezishutumu Eritrea na Misri kwa kuchochea maandamano hayo.
2. Vyombo vya habari
Huwezi kutazama vituo vya Esat na OMN vya televisheni, vilivyo na makao yake nje ya nchi. Serikali imezitaja kumilikiwa na 'makundi ya kigaidi'.
3. Maandamano
Kumeshuhudiwa maandamano katika miezi ya hivi karibuniImage copyrightREUTERS
Image captionKumeshuhudiwa maandamano katika miezi ya hivi karibuni
Huwezi kupanga mandamano shuleni au katika chuo kikuu unakosoma, na hakuna ruhusa ya kuwa mfuasi wa kampeni ya kisiasa ambayo huenda 'ikazusha ghasia, chuki, na ukosefu wa imani miongoni mwa raia'.
4. Ishara
Mwanariadha Feyisa Lilesa alikunja mikono hewani katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu - ishara ya maandamano ya Oromo inayotambulika kote dunianiImage copyrightAFP
Image captionMwanariadha Feyisa Lilesa alikunja mikono hewani katika mashindano ya Olimpiki mwaka huu - ishara ya maandamano ya Oromo inayotambulika kote duniani
Huwezi kuonyesha ishara ya kisiasa, kama kukunja mikono juu ya kichwa au kuwasilisha ujumbe wa kisiasa kwa umma 'bila ya ruhusa'.
Ishara hiyo ya kukunja mikono imetumika pakubwa katika maandamano ya Oromo na pia katika mashindano ya Olimpiki Rio de Janeiro mnamo Agosti.
5. Marufuku ya kutotoka nje
Viwanda vimelengwa katika maandamano EthiopiaImage copyrightREUTERS
Image captionViwanda vimelengwa katika maandamano Ethiopia
Huwezi kutembelea kiwanda, shamba au taasisi ya serikali kati ya saa kumi na mbili jioni hadi kumi na mbili alfajiri. Ukikiuka marufuku ya kutotoka nje, 'vikosi vya sheria vimeagizwa kuchukua hatua zipasazo'.
6. Wanadiplomasia
Gari la kidiplomasiaImage copyrightAFP
Kama wewe ni mwanadiplomasia hauruhusiwi kusafiri zaidi ya kilomita 40 kutoka mji mkuu Addis Ababa, bila ya ruhusa. Serikali inasema ni kwa usalama wako.
Kwa jumla hakujatolewa tamko lolote kidiplomasia kuhusu hali ya tahadhari ilioidhinishwa.
7. Bunduki
Kama unamiliki bunduki, huwezi kuibeba kufikia kilomita 25 za barabara kuu za mji mkuu Addis Ababa, na kufikia kilomita 50 za mipaka ya nchi hata kama una kibali cha umiliki.

Taarifa zaidi kuhusu maandamano ya Ethiopia

Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles