» »Unlabelled » Lesson ya Wiki him somo Laana Bila Sababu?

Laana Bila Sababu?

SABATO MCHANA

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili:Zab. 119:65-72Ayubu 2:11-13Ayubu 4:1-21Warumi 3:19, 201 Wakorintho 3:19Waebrania 12:5Mathayo 7:1.

Fungu la Kukariri: “Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu? Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?”(Ayubu 4:17).

Juma lililopita tulisisitiza umuhimu wa sisi kujiweka katika nafasi ya Ayubu, angalau kwa kiasi cho chote kinachowezekana. Kwa namna moja tu, isingekuwa vigumu kufanya hivyo, kwa sababu sisi sote tumewahi kuwa katika mazingira kama hayo; yaani, kwa kiasi fulani kila mmoja wetu amewahi kujikuta katika mateso ambayo mara nyingi yanaonekana kutokuwa na sababu na bila shaka huonekana kwamba hayastahili.

Huku tukiendelea kuyaangalia mambo katika mtazamo huohuo katika sehemu iliyobakia ya somo hili, tunatakiwa pia kuangalia mtazamo wa watu wengine katika kisa hiki, wale waliokuja kuomboleza na kusikitika pamoja na Ayubu. Hata hilo halipasi kuwa jambo gumu. Ni nani kati yetu ambaye hajawahi kuona mateso ya wengine? Ni yupi kati yetu ambaye hajawahi kujaribu kufariji watu wengine walio katika uchungu na misiba? Ni nani asiyejua ilivyo kutafuta maneno sahihi ya kuzungumza na wale ambao masononeko yao yanaiumiza pia mioyo yetu wenyewe?

Kusema kweli, sehemu kubwa ya kitabu cha Ayubu ni mazungumzo kati ya Ayubu na watu hawa, wakati wote kwa pamoja wakijaribu kutafuta maana ya kile ambacho mara nyingi huonekana kutokuwa na maana: Mfululizo usio na mwisho wa mateso ya wanadamu na majanga yaliyo katika ulimwengu ulioumbwa na Mungu mwenye upendo, mwenye nguvu na anayejali.

*Soma juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya Novemba 5.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles