» »Unlabelled » *K E S H A LA A S U B U H I* IJUMAA-OCT-28/2016

*K  E   S   H  A   LA   A S U B U H I*
IJUMAA-OCT-28/2016

🍃🌿🍃🌿🍃🌿🍃🌿

*NENO KUU 👇🏽*

*_TUNAKAA NDANI YA KRISTO 👇🏽_*

*👉🏽Walioshutumiwa Wanabarikiwa*

*Fungu la maandiko 👇🏽*

*_👉🏽📝Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu._*   *Mathayo 5:11.*

🍇🌹🍇🌹🍇🌹🍇🌹

    *_➡Hakujawahi kuwepo mtu aliyeishi kati ya watu ambaye alikashifiwa zaidi ya Mwana wa Adamu. Alibezwa na kudhihakiwa kwa sababu ya utiifu wake ambao haukuyumba katika kanuni za sheria ya Mungu iliyo takatifu. Walimchukia bila sababu. Na bado alisimama kwa utulivu mbele za adui zake, akitamka kwamba shutuma ni sehemu ya urithi wa Mkristo, akiwashauri wafuasi wake namna ya kukabiliana na vijicho, akiwasihi wasichoke katika mateso._*

         *_➡Ingawa kashfa inaweza kuchafua sifa, haiwezi kuweka doa katika tabia. Hiyo ipo katika uangalizi wa Mungu. Kadiri tunavyokataa kukubali dhambi, hakuna nguvu, iwe ya kibinadamu au ya Kishetani, inayoweza kutia nafsi doa. Mtu ambaye moyo wake unadumu kwa Mungu ni yule yule katika saa ya majaribio ya makali zaidi na mazingira yanayokatisha tamaa sana, kama alivyo wakati wa mafanikio, wakati nuru na wema wa Mungu unapoonekana kuwa juu yake. Maneno yake, makusudio yake, matendo yake, vinaweza kutowasilishwa ilivyo sahihi na kupewa mwonekano wa uongo, lakini yeye hatajali hilo, kwa sababu anawajibika kwa ajili ya maslahi ya juu zaidi. Kama Musa alivyokuwa, atastahimili “kama amwonaye yeye asiyeonekana.”…_*

     *_➡Kristo anajua yote yanayoeleweka vibaya na kupotoshwa na watu. Watoto wake wanaweza kungoja kwa subira na matumaini yenye utulivu, bila kujali wanatengwa na kudharauliwa kiasi gani; kwani hakuna kilicho sirini ambacho hakitadhihirishwa na wale wanaomheshimu Mungu wataheshimiwa na yeye mbele za watu na malaika._*

     *_➡“Thawabu yenu ni kubwa mbinguni” kwa ajili ya wale walio mashahidi wa Kristo kupitia katika mateso na shutuma. Watu wanapokuwa wakitafuta vitu vya kidunia, Yesu anawaelekeza kwa thawabu ya kimbingu. Lakini haiweki yote katika maisha yajayo; inaanzia hapa._*

……………………🔚…………………………

*U    B    A     R    I   K   I    W   E*


🌹🍇🙇🏻

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles